WAKULIMA KUFAIDI NA MBOLEA NA NYASI KUTOKA KWA SERIKALI YA KAUNTI YA UASIN GISHU

You are currently viewing WAKULIMA KUFAIDI NA MBOLEA NA NYASI KUTOKA KWA SERIKALI YA KAUNTI YA UASIN GISHU
  • Post category:Biashara

Wakulima Kaunti ya Uasin gishu kupitia vyama vyao vya ushirika watafaidi na mbolea pamoja na nyasi kutoka kwa serikali ya Kaunti hiyo zoezi ambalo linalenga wakulima 200.

Hii ni baada ya uongozi wa Kaunti hiyo kupanga kutoa mbegu ya nyasi ambayo inaambatana na mbolea yake ili kukuza uzalishaji zaidi wa maziwa sawa na kuinua mapato na uchumi wa wafugaji wa ngome wa maziwa.

Aidha wakulima wamekaribisha hatua hiyo kutokana na kwamba wamekumbwa na changamoto nyingi hususani wakati wa kiangazi na kupitia mpango wa serikali ya kaunti hiyo watafaidi na ufugaji.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.