Wakulima katika shamba la Natot liliko kaunti ndogo ya Turkana ya kati wanakadiria hasara baada ya mazao yao kusomba na mafuriko kutokana na mvua inayoendelea kunyesha kaunti hiyo.
Kulingana na Mshirikishi wa miradi ya jamii katika Shirika la Right Hope International liliko kaunti ya Turkana Victor Juma, zaidi ya familia 74 sasa watakosa chakula kufuatia uharifu ambao umesababisha na mafuriko hasa wakulima.
Aidha Juma anasema mradi huo umeharibiwa pakubwa na itakuwa vigumu kwa wakulima kuendeleza kilimo cha mimea ili kuwasaidia wakaazi wa kaunti ya Turkana kupata chakula.
Hata hivyo ametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Turkana na wahisani kujitokeza kupiga jeki mradi huo ambao kwa sasa umeharibiwa na mafuriko ili kusishuhudiwe na uharibifu zaidi.