Wakazi wa mtaa wa mabanda ya Kipsongo na Matisi wameirai uongozi wa Kaunti ya Trans Nzoia, kujenga vyoo vya umma ili kuzuia hali ambapo baadhi yao huenda haja kubwa katika vichaka karibu na mto Kipsongo.
Wakazi hao wakiwemo, Ruth Musundi na Fred Bunguswa wanahofia kwamba huenda uchafu huo ukachanganyika na maji ya mto na kusababisha wao kuugua maradhi ya kipindupindu msimu wa mvua kubwa.
Kwa upande wake mkazi wa mtaa huo, Janet Silali amesema vichaka hivyo vinawaweka watoto wa kike katika hatari ya kudhulumiwa kingono.