WAKAZI TURKANA WALALAMIKIA UKATILI UNAONDELEZWA NA POLISI

  • Post category:County News

Wakaazi wa mji wa lodwar kaunti ya Turkana wamelalamika kunyanyaswa na maafisa wa usalama ambao wanaendelea kutekeleza amri ya kutotoka nje kaunti hiyo. 

Wakizungumza mjini Lodwar wakaazi hao wakiongozwa na John Ereng wamesema wametamahushwa na vitendo vya polisi kuwadhulumu wananchi na kupora mali zao kwa kisingizio cha kutekeleza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku wakati serikali imewapa jukumu la kulinda  usalama wao.

Lalama zao zinakuja baada ya maafisa wa polisi kuvunja duka moja mjini lodwar na kupora shilingi alfu hamsini pamoja na kadi ya muda wa maongezi yenye dhamana ya shilingi alfu kumi.

Aidha wakazi hao wametoa wito kwa Inspekta Jenerali wa polisi Hillary Mutyambai kuingilia kati na kuzuia ukatili unaoendelezwa na vyombo vya usalama kwani kwa sasa wanaishi kwa hofu.

Hata hivyo wakuu wa idara ya usalama kaunti ya turkana wamekiri kupokea lalama hizo na wameanzisha uchunguzi dhidi ya tuhuma ambazo wananchi wamezielezea.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya