wakaazi wa wadi ya Lodwar Township wamemtaka mwakilishi wa wadi wa eneo hilo Robert Lowoko kuivunja kamati ya usimamizi wa fedha za basari kwa madai ya kufuja shillingi millioni 5 iliyotengwa kufadhili masomo ya wanafunzi wasiojiweza.
Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Lodwar wakaazi wa wadi ya Lodwar Township wameulamu uongozi wa kamati ya fedha ya hazina ya masomo wakisema kuwa wanatumia vibaya afisi yao kutoa pesa za basari kwa njia ya ubaguzi.
Aidha wakaazi hao wamesema nia yao ni kupinga uovu unaoendelea katika usimamizi wa afisi ya mwakilishi huyo wa wadi ambao umekuwa ukitatiza ugavi sawa wa fedha za basari ikizingatiwa kuwa watoto 100 pekee kati ya 900 kutoka familia maskini ndio walikuwa wamefaidi.
Hata hivyo mwakilishi wadi wa Lodwar Township Robert Lowoko ameivunja kamati iliyokuwa ikisimamia basari wadi hiyo huku akitupilia mbali orodha ya wanafunzi walioteuliwa kufaidi na mgao wa shillingi millioni 5 za basari na kuahidi kubuni kamati nyingine ambayo itaendesha zoezi la kugawa basari kwa usawa.