WAKAAZI WA TURKANA WATAKIWA KUFUATA KANUNI ZA AFYA KUHUSU COVID-19

Wakaazi wa kaunti ya Turkana wametakiwa kufuata taratibu na kanuni zinazotolewa na serikali kupitia wizara ya afya kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya COVID-19 nchini.

Akizungumza kwenye misa ya Wafanyikazi wa jimbo katoliki la Lodwar iliyofanyika mjini Lodwar, Msimamizi wa Afya  kaunti ndogo ya Turkana ya kati Bwana Lumbasi Rabando amesema kila mkaazi lazima azingatie taratibu husika ili kuzuia maambukizi zaidi.

Aidha Rubando amewaonya wakazi  wa kaunti ya turkana dhidi ya kupuuza maagizo ya kuzuia maambukizi ya corona.

Kauli yake inakuja baada ya watu watatu wanaohudumu jimbo katoliki la Lodwar kukutwa na virusi vya Covid-19 na kuweka karantini.

Ikumbukwe Serikali ya kaunti ya Turkana imekuwa ikiwahimiza wakazi wa kaunti hiyo kufuata maagizo ya afya ya umma ikiwemo kuvaa barakoa, kuosha mikono na kutotangamana ila wakazi wengi wamekuwa wakisusia maagizo hayo.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa