Wakaazi wa kaunti ya Turkana wametakiwa kujitenga na kadhia ya kutimia mitandao ya kijamii kueneza taarifa za hofu kuhusiana na ugonjwa wa Corona ambao unaendelea kutikisa dunia.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa Afya kaunti ya Turkana jane ajele amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kutokuwa na hofu ya corona wakati huu ambapo kamati iliyobuniwa kushugulikia maambukizi ya Corona inaendelea na wajibu wake.
Aidha Ajele ametoa wito kwa wakaazi wa kaunti ya Turkana kuzingatia usafi kwa kunawa mikono kila mara kwa maji safi yanayotiririka na vitakasa (sanitizers) ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
Kauli ya Ajele inakuja baada ya raia mmoja wa uchina aliyeshukiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa corona kufanyiwa vipimo na kubainika kuwa hana ishara zozote za ugonjwa huo.