WAKAAZI WA SACHO KAUNTI YA BARINGO WAANDA IBADA MAALUM KUMKUMBUKA HAYATI MZEE MOI

Huku shughuli ya kuutazama mwili wa hayati mzee Daniel Toroitich Arap Moi ukitamatika leo, wakaazi kutoka wadi ya Sacho, Baringo ya Kati wameandaa maombi kwa minajili ya familia ya mzee Moi.

Kufuatia mapendekezo ya umma, kutaka mwili wa mzee Moi usafirishwe kaunti ya Baringo ili waweze kuutazama, Clint Kiprono Moi, mjukuu wa mzee moi amesema ombi hilo sasa haliwezekani kwani mipango ya mazishi kwa sasa inaendeshwa na serikali kuu na hivyo wao kama kama familia wanatazama na kufuatilia matukio kwenye runinga kama wakenya wengine.

Aidha Kamishna wa kaunti ya Nyandarua Boaz Cherutich amesema wakaazi wa kaunti ya Baringo watafuatilia mazishi ya mzee moi kwenye runinga vitakavyotundikwa kwenye maeneo ya Sacho, Kabarnet na Eldama Ravine

Kwa upande wake karani wa Bunge la kaunti ya Baringo Richard Koech amesema kuwa wanajivunia maendeleo kama shule na barabara kwa heshima ya marehemu mzee Moi.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts