Wakaazi wa Narewa wadi ya Kanamker kaunti ndogo ya Turkana ya Kati wameandamana kulalamikia kampuni ya ujenzi ya China Railway 5 kwa ujenzi mbaya wa bomba la kupitisha maji taka ambalo huenda likaathiri shughuli zao.
Wakaazi hao wakiongozwa na mzee Calis Emanikor ambaye ni mzee wa kijiji cha Narewa,kilichoko wadi ya Kanakemer wamesema hawataruhusu kampuni hiyo iendelee na shughuli ya ujenzi wa barabara katika eneo hilo hadi pale serikali ya kaunti itakaposikiliza lalama zao.
Aidha wamesema eneo hilo linakumbwa na uhaba mkubwa wa maji jambo ambalo wamesema limeathiri suala nzima la kupambana na janga la corona.
Hata hivyo mtawala wa wadi ya Kanamkemer Shaban Etabo amewataka wakaazi hao wawe na subira wakati huu uongozi wa wadi hiyo unashughulikia matakwa yao.