WAKAAZI WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WANUFAIKA NA VIFAA VYA KUIMARISHA LISHE KUTOKA KWA SHIRIKA LA AMREF NA MASHIRIKA MENGINE

You are currently viewing WAKAAZI WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WANUFAIKA NA VIFAA VYA KUIMARISHA LISHE KUTOKA KWA SHIRIKA LA AMREF NA MASHIRIKA MENGINE

Shirika la Utafiti wa Kiafya Barani Afrika Amref likishirikiana na Umoja wa Ulaya na mashirika mengine manne yakiwamo Shirika lisilokuwa la Kiserikali la NRT chini ya mpango wa Ustahimilivu limezuru Kaunti ya Pokot Magharibi kuwapa Wakazi vifaa vya kuimarisha Lishe pamoja na vifaa vingine vya kuboresha Usafi wa Maji na Vyakula.

Mshirikishi mkuu wa shirika la Amref Esther Wambui anasema wamekuja pamoja na mashirika mengine ili kuhakikisha wanapiga vita matatizo ya lishe bora miongoni mwa Watoto katika Kaunti ya Pokot Magharibi.

Wambui ametaja hali ya Watoto kudhohofika Kiafya kutokana na ukosefu wa lishe bora kuwa changamoto kubwa inayowakumba Watoto wengi katika Kaunti hiyo, huku akisema Utafiti wa Shirika hilo linaonyesha kwamba Kaunti ina asilimia thelathini na tano nukta moja ya Watoto waliodumaa kutokana na changamoto za Kiafya.

Waziri wa afya Jack Yaralima ameyarai Mashirika mengine pamoja na wahisani kupiga jeki juhudi za Serikali ya Kaunti ya Pokot Magharibi kukabili matatizo ya Kiafya miongoni mwa Watoto wachanga.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.