WAKAAZI WA KABIMOI KAUNTI YA BARINGO WAMETAKA KUHUSISHWA KWENYE HAFLA YA MAZISHI YA HAYATI MZEE MOI

Wakaazi wa lokesheni ya Kabimoi, eneo bunge la Eldama Ravine kaunti ya Baringo wameitaka serikali kutambua eneo hilo kwenye sherehe za kumuaga Rais mstaafu hayati mzee Daniel Toroitich Arap Moi kwani Kabimoi ilikua makaazi ya mzee Moi alipokuwa Naibu wa rais wa taifa la Kenya.

Wakiongozwa na Michael Kandie  na Isaac Noriega wamependekeza sherehe ya kumuaga mzee Moi kufanyika katika eneo la Kabimoi sambamba na ile itafanyika nyumbani kwake  Kabarak kwa heshima yake.

Wakati huo huo aliyekuwa wakati mmoja Diwani wa Eldama Ravine zamani ikifahamika kama Baraza la wilaya ya Koibatek Abdul Musa ameunga mkono kauli hiyo, huku akiwaponda wananchi wanaosema serikali imefeli kuuleta mwili wa hayati mzee Moi kuutazamwa  katika kaunti ya Baringo akisema mzee moi alikuwa kiongozi wa taifa nzima na hafla hiyo kuandaliwa jijini Nairobi ni kuzipa fursa makabila na tabaka zote kumpa heshima za mwisho mzee Moi

Ikumbukwe kuwa zoezi la siku tatu la kuutizama mwili wa marehemu Daniel Toroitich Arap Moi limekamilika leo ambapo wananchi kutoka maeneo tofauti nchini walipata fursa ya kumpa  heshima zao za mwisho katika majengo ya bunge kabla ya kuandaliwa kwa misa ya kitaifa ya mazishi hapo kesho katika uwanja wa Nyayo Jijini Nairobi na mazishi kuandaliwa siku ya jumatano nyumbani kwake Kabarak kaunti ya Nakuru.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts