WAKAAZI WA CHERANGANY WAMEMKASHIFU MBUNGE WA KIMILILI CHRIS WAMALWA KWA MADAI YA KUZUA VURUGU KWENYE HAFLA YA MAZISHA ENEO HILO

Viongozi wa makanisa pamoja na vijana wameshtumu siasa zilizosheheni katika mazishi ya mamake wakili Benson Milimo eneo bunge la Cherangany ambapo viongozi walitofautiana hadharani kuhusiana na yule anayetakiwa kugombea kiti cha ugavana wa kaunti hiyo mwaka wa 2022

Mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa alionekana kukerwa na madai yaliyoibuliwa na mshauri wa Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa kuwa waziri huyo atawania ugavana  kaunti ya Trans-Nzoia kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022, akisema yupo tayari kukabiliana na naye.

Ni hatua ambayo imekashifiwa na viongozi wa makanisa wakiongozwa na Albert Nyasetia pamoja na vijana wa eneo hilo huo wakiapa kuwa wataandaa maandamano ya kushinikiza Chris Wamalwa achukuliwe hatua kali za kisheria

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts