WAKAAZI TURKANA WAMETAKIWA KUKUMBATIA MPANGO WA HUDUMA ZA BIMA KWA MIFUGO

WAKAAZI TURKANA WAMETAKIWA KUKUMBATIA MPANGO WA HUDUMA ZA BIMA KWA MIFUGO

Wito umetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Turkana kuwandikisha mifugo wao katika mpango wa serikali wa huduma za bima ya mifugo ili kuwaepusha na athari ya ukame.

Akizungumza kwenye warsha ya siku mbili mjini Lodwar, mshirikishi wa mpango wa serikali wa kutoa huduma ya bima kwa mifugo Dakta Richard Kyuma amesema mpango huo utasaidia kukabiliana na hatari za ukame zinazowakabili mifugo kwani itaboresha maisha ya wakulima na jamii za wafugaji.

Kauli sawa imetolewa na waziri wa kilimo kaunti ya turkana Chris Alete ambaye amesema huduma ya bima kwa mifugo itapunguza hali ya wakaazi wa kaunti hiyo kutegemea chakula ya misaada mbali na kukuza biashara ya mifugo kwa maslahi yao kiuchumi.

Hata hivyo mpango wa serikali wa huduma ya mifugo KLIP ulianzishwa mwaka wa 2014 ili kulinda jamii za wafugaji dhidi ya maafa ya ukame hasa katika kaunti 14 zinazokumbwa na ukame mara kwa mara na tangu kuanzishwa kwake umewafaidi takriban wafugaji 32,000 kote nchini.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts