Baada ya Tume ya Uchaguzi nchini kuidhinisha saini za kuunga mkono mchakato mzima wa BBI na kuzitaka Mabunge ya Kaunti kujadili mswada huo, baadhi ya wakaazi wa Kaunti ya Pokot Magharibi wametoa hisia zao kuhusu iwapo wawakilishi wadi wataidhinisha mswada huo.
Wakizungumza na kituo hiki, wakaazi hao wanasema Mabunge ya Kaunti hayana budi kupitisha mswada huo wa kufanyia katiba marekebisho kwani serikali za kaunti zitafaidi pakubwa huku baadhi wakisema mwananchi wa kawaida atabebeshwa mzigo mzito.
Haya yanajiri huku kampeni za kupigia debe mchakato wa BBI ukielekezwa eneo la Mlima Kenya, ambapo Rais Uhuru Kenyatta amezuru eneo hilo kuwashawishi wakaazi na viongozi kuunga mkono huku Mabunge ya Kaunti yakitarajiwa kuipa kipaumbele mswaada huo baada ya likizo ndefu.