WAIDHISHWA NA WIZARA YA AFYA KUWA BORA KWA KUMILIKI VYOO

WAIDHISHWA NA WIZARA YA AFYA KUWA BORA KWA KUMILIKI VYOO

Eneo la Locher Ekuyen iliyoko kaunti ndogo ya Loima imeidhinishwa na wizara ya afya kaunti ya turkana kuwa miongoni mwa maeneo ambayo wakaazi wake wamekumbatia matumizi ya vyoo.
Mshirikishi wa kitengo cha Wash unit katika kaunti ya turkana Reuben Kibiego amesema uamuzi huo umetokana na hatua ya makaazi 750  ambayo yapo eneo hilo kumiliki vyoo.
Aidha Kibiego amesema mpango wa huo wa usafi kupitia matumizi ya vyoo ulianzishwa mwezi mmoja uliopita na wizara ya afya kaunti pamoja shirika la Unicef lilenga kuhakikisha wakaazi wanaoishi eneo la Locher Ekuyen wanaepukana na mkurupuko wa mangonjwa yanayotokana na uchafu.
Hata hivyo eneo la locher Ekuyen inajiunga na maeneo mengine bora 50 ambayo tayari yameidhishwa kuwa maeneo ambayo yamekubatia matumizi ya vyoo kwenye kaunti ya turkana.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts