WAFANYIBIASHARA TURKANA WAAHAPA KUTOLIPA USHURI KUTOKANA NA MAZINGIRA DUNI YA SOKO KUU LA LODWAR

Wafanyibiashara katika soko kuu la Lodwar kaunti ndogo ya Turkana ya kati wameapa kutotozwa ushuru hadi serikali ya kaunti ya Turkana itakapofanya maendeleo katika soko hilo.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Peter Areman wafanyibiashara hao wamedai soko kuu la Lodwar limebaguliwa na serikali ya kaunti hiyo licha ya wao kulipa ushuru kwa wakati.

Aidha wamekashifu hatua ya serikali ya kaunti kutumia vyombo vya usalama kuwalazamisha wafanyibiashara kulipa ushuru ilhali mazingira wanayofanyia biashara ni duni.

Hata hivyo wafanyibiasha hao kwa kauli moja wameapa kuandaa maandamano kila wiki hadi pale serikali ya kaunti ya Turkana itakarabati soko hilo.

Miongoni mwa yale wafanyibiashara hao wanahitaji yafanywe katika soko hilo ni kujengwa kwa vyoo vipya, kukarabatiwa kwa mabomba ya maji taka, na kuhimarisha kwa usalama m  iongoni mwa mahitaji mengine.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts