WADAU WA ELIMU TURKANA WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA KUBORESHA VIWANGO VYA ELIMU

Viongozi kutoka kaunti ya Turkana wametoa wito kwa washikadau katika sekta ya elimu kuweka mikakati ya kuboresha viwango vya elimu katika eneo hilo.

Wakiongozwa na Gavana wa kaunti ya Turkana Josphat Nanok, wamesema kuwa ni jambo la kufedhehesha kuona shule nyingi za msingi na upili zikifanya vibaya kwenye mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE.

Kauli sawa imetolewa na Naibu Gavana Peter Lotethiro ambaye amewataka  walimu, wazazi na viongozi wengine kuweka mawazo yao pamoja na kutafuta suluhu kwa tatizo hilo.

Wakati huo huo  Mbunge wa Turkana ya kati John Lodepe amewataka wazazi kushirikiana na wadau wa elimu wakiwemo wahisani kwa lengo la kuboresha na kuimarisha viwango vya elimu maeneo hayo.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts