WAATHIRIWA WA MAPOROMOKO YA ARDHI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAPOKEZWA MAKAAZI MAPYA

WAATHIRIWA WA MAPOROMOKO YA ARDHI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAPOKEZWA MAKAAZI MAPYA

Zaidi ya shilingi milioni 25 zilitumika katika ujenzi wa makaazi ya watu 223  walioathirika na maporomoko ya ardhi eneo la Nyarkulian, Tamkal na Muino mwaka jana.

Akizungumza alipofungua rasmi makaazi hayo gavana wa Pokot Magharibi  John Lonyangapuo amesema watu wengine wawili hawajajengewa nyumba hizo kutokana na ujeuri wao akisema kwamba pesa zao zimetengwa.

Aidha Lonyangapuo amewaonya wale wanaoeneza propaganda kuhusu matumizi ya pesa zilizotengewa waathiriwa wa mkasa huo akisema uongozi wake umeendesha shughuli nzima kwa uwazi.

Wakati huo huo katika mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Asha Mohammed ameahidi kuendeleza ushirikiano na serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi kwa kuhakikisha walioathirika na mkasa wa mafuriko eneo la Chesegon pia wanapata msaada ili na wao pia waweze kuendeleza maisha yao

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya