WAANDISHI WA HABARI TURKANA WALAANI TUKIO LA MWENZAO KUSHAMBULIWA

Wanahabari wanaohudumu kwenye kaunti ya Turkana wamekilaani kitendo cha wafanyikazi wa hoteli moja mjini lodwar kumvamia na kumjeruhi vibaya mwahandishi wa gazeti la star, wakikitaja kitendo hicho kama cha kuingilia uhuru wa vyombo vya habari katika utendakazi wao.

Katika taarifa wahandishi hao  wakiongozwa na Philip Ekadeli na mwenzake wa Shirika la The  Standard Bakari Angela wamesema wahudumu wa hoteli hiyo walikiuka sheria za kitaifa na kimataifa za wanahabari kupata habari na hivyo basi waliohusika katika kitendo hicho wanapaswa kuadhibiwa.

Wakati huo huo Hesboun Etyang ambaye ni mwanahabari wa gazeti la the star aliyejeruhiwa vibaya na wafanyikazi wa hoteli ya stegra, ameeleza kuwa licha ya yeye kujitambulisha wakati alipokuwa akipiga picha tukio la mtoto wa miaka kumi na miwili kuzama ndani ya kidimbwi cha maji hoteli humo, wahudumu hao walimpiga na kuharibu vyombo vyake vya kazi.

Hata hivyo wanahabari kaunti ya turkana kwa kauli moja wameshinikiza kufutwa kazi kwa wafanyikazi waliohusika kwenye purukushani hiyo na kushtakiwa kwa makosa ya kuwashambulia na kumtesa mwanahabari mwenzao.

Wakati Huo huo Baraza la vyombo vya habari nchini media council limetamaushwa na kitendo cha kushambuliwa kwa mwandishi wa gazeti la the star anayehudumu kaunti ya turkana.

Meneja wa mipango katika baraza hilo Victor Bwire amesema kuwapiga na kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi yao ni kinyume cha katiba, akiwataka waandishi wa habari kuwa makini katika kazi zao na kuchukua tahadhari ili kujikinga na hatari zozote zinazoeza kutokea.

Kauli sawa imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maripota William Oloo Janak akikashifu kitendo cha   wafanyikazi wa hoteli ya Stegra kumshambulia mwanahabari huyo na kuitaka idara ya upelelezi na ile ya mashtaka ya umma nchini kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika katika kitendo hicho.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts