Viongozi kutoka katika kaunti ya Turkana wameonyesha wasiwasi wao kutokana na ongezeko la visa vya ukosefu wa usalama katika baadhi ya sehemu za kaunti hiyo hasa zile zinazopakana na nchi ya sudan kusini na Ethiopia.
Akizungumza mjini lodwar Mbunge wa Turkana Magharibi Daniel Epuyo amesema wakaazi wanaoishi mpaka mwa nchini hizo wamepoteza maisha yao huku akitaka serikali kuwatuma maafisa zaidi ya usalama kushika doria katika eneo hilo kwani wenyeji wanaisha na hofu ya kushambuliwa na magaidi.
Kwa upande wake mbunge wa Loima Jeremiah Lomurkai ameitaka serikali kuu kuendesha operasheni inayoendelea mpakani mwa kaunti ya Turkana na Baringo bila upendeleo hadi pale majangili wanaotatiza amani eneo hilo watakaposalimia amri.