VIONGOZI MLIMA ELGON WAMEMMINIA SIFA HAYATI MZEE MOI KWA KUWEKA MASLAHI YA MAENDELEO MBELE.

Huku taifa likiendelea kuomboleza kifo cha  hayati mzee Daniel Toroitich Arap Moi baadhi ya viongozi kutoka eneo bunge la Mlima Elgon waliohudumu wakati wa utawala wa kiongozi huyo wameelezea kutamaushwa  na kifo chake wakimtaja kama  kiongozi aliyejali maslahi ya wakaazi wa eneo hilo.

Wakiongozwa na Francis Burko aliyehudumu kama diwani wakati wa utawala wa hayati mzee Moi, wamesema watamkumbuka kwa mengi aliyowafanyia wakaazi wa Mlima Elgon yakiwemo kuipa elimu kipaumbele kando na kuwahimiza kukumbatia chama cha KANU.

Kwa upande wake  James Maruka mwanaharakati wa kisiasa eneo hilo amesema upendo wa Moi kwa wenyeji wa Mlima Elgon ulidhihirika waziwazi kwani alikuwa anapenda kutembelea eneo hilo mara kwa mara kando kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile kuanzisha kilimo cha Chai  maarufu Nyayo Tea Zone.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts