VIFAA VYA MATIBABU VILIVYOSAMBAZA NA WIZARA YA AFYA KWENYE HOSPITALI YA RUFAA NA MAFUNZO YA MOI HAVIFANYIKAZI

Imebainika kuwa asilimia kubwa ya vifaa vya matibabu katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya moi mjini eldoret havifanyikazi.

Seneta wa isiolo Fatuma Dullo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati maalum ya seneti ambayo inachunguza sakata ya vifaa vilivyosambazwa na wizara ya afya amesema hata baada ya hospitali hiyo kupokea vifaa asilimia kubwa ya vifaa hivyo havifanyikazi.

Wakati huo huo seneta wa kaunti ya Uasin Gishu Profesa Margaret Kamar ametaja swala la ukosefu wa wataalamu wa kutumia vifaa hivyo kama changamoto ambazo zimelemaza utoaji wa hudumu bora kwa wenyeji.

Kwa upande wake Afisa mkuu mtendaji wa Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi Wilson Aruasa amesema huduma za matibabu zinazotolewa katika hospitali ya nyingi kaunti hiyo hazipendezi kutokana na ukosefu wa madaktari wa kutosha

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts