Socialite maarufu nchini ambaye pia ni mfanyibiashara Vera Sidika amepuzilia mbali madai yanayotembea kwenye mitandao kuwa amejishusha hadhi baada ya kukubali kuingia kwenye ndoa na msanii wa muziki nchini Brown Mauzo.
Akijibu maswali ya mashabiki zake kwenye mtandao wa instagram Vera Sidika amenyosha maelezo kuhusiana na suala hilo kwa kusema kuwa pesa haijekuwa kigezo cha yeye kuingia kwenye mahusiano kwa sababu awali alikuwa kwenye mahusiano na watu wenye mkwanja mrefu, hivyo mambo hayakuwa mazuri kama jinsi watu wanavyodhani.
Bi sidika ameenda mbali zaidi na kusema kuwa hayuko tayari kuharibu furaha na uhuru wake kwa kuingia kwenye mahusiano na matajiri kwa ajili ya pesa.
Hii si mara ya kwanza kwa mrembo huyo kudai yupo katika penzi zito na msanii wa muziki nchini kwani kipindi cha nyuma alitangaza wazi kuwa amefunga ndoa na msaani Otile Brown lakini baadae walikuja wakaachana.