UONGOZI WA CHUO CHA TURKANA UMEKANA MADAI YA KUWEPO MZOZO WA UONGOZI CHUO HUMO

Uongozi wa Chuo kikuu cha Turkana umepuzilia mbali taarifa zilizokuwa zikienezwa kuwa kuna mzozo wa uongozi chuoni humo.

Katika taarifa kwa Vyombo vya habari,Kaimu Mwalimu mkuu wa chuo hicho Professa Tom  Nyamacha ambaye anashikilia wadhfa  wa Professa Stephen Odebero ambaye yupo ziarani nchini Austria, amesema aliyekuwa mwalimu mkuu wa chuo cha Turkana  Professa Thomas Akuja alitumwa likizo ya lazima kutokana na matumizi mabaya ya mamlaka.

Aidha Nyamacha amesema shughuli za masomo zinaendelea kama kawaida katika chuo hicho licha ya lalama ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Turkana.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts