Kwa mujibu wa tathmini iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la UNICEF, imeelezwa athari kubwa za janga la COVID-19 kwa Wanawake katika baadhi ya Mataifa huenda zikasababisha zaidi ya Ndoa Milioni 10 za Watoto katika muongo huu.
Kufungwa kwa Shule, msongo wa kiuchumi, kuvurugwa kwa huduma na vifo vya Wazazi kutokana na COVID-19 vinawaweka Wasichana katika mazingira hatarishi zaidi ikiwemo kuozeshwa wakiwa wadogo.
Mwelekeo huo ikiwa utathibishwa, utasababisha kurudi nyuma zaidi mafanikio ya miaka kadhaa dhidi ya ndoa za Watoto. Miaka 10 iliyopita, kiwango cha Wasichana walioolewa wakiwa Watoto kilipungua kwa asilimia 15, kutoka mmoja kati ya wanne hadi mmoja kati ya watano.