Kiongozi wa Upinzani Nchini Uganda, Robert Kyagulanyi ametoa wito kwa Wananchi kuandamana kwa Amani na bila silaha kumpinga Rais Yoweri Museveni aliyetawala Taifa hilo kwa karibu miongo minne.
Akizungumza akiwa Makao Makuu ya Chama cha National Unity Platform (UNP) mjini Kampala, Wine amesema muda umefika kwa Umma kuandamana dhidi ya Museveni aliyeingia rasmi Madarakani mwaka 1986.
Jeshi la Polisi limeonya kuhusiana na wito huo na kusema halitasita kumkamata na kumfungulia mashitaka yeyote atakayeshiriki maandamano na shughuli zozote kinyume cha Sheria.