Twitter imekuwa ikitafuta namna nyingine ya kupata faida kwa kuweka huduma za malipo au subscription kwa watumiaji. Mafanikio ya majaribio yake yamefanikiwa na wiki hii Twitter imetambulisha huduma ya Super Follow.
Super Follow, ni mfumo ambao watumiaji wataweza kulipia kwa mwezi kupata Tweets, kupata badges, Audio chats, na DMs za kiupekee.
Hii italeta faida kwa watumiaji wa Twitter ambao watapata faida kwa kutoa tweets na content za ziada ambazo followers watalipia kila mwezi kuzipata. Mabadiliko haya yataenda kubadilisha sana mfumo wa Twitter.
Bei ya mwanzo itakuwa ni dollar 4.99 ambazo ni sawa na shilingi 546.90 za Kenya. Inaweza kuleta faida kubwa kwa wasanii, watu maarufu wa Twitter kupata faida kwa kuweka content za kiupekee.
Pia Twitter inafanya majaribio ya kuweka communities kama ilivyo Facebook groups ila bado twitter haijasema muda maalum wa kuweka maboresho hayo lakini imetambulisha ujio wa huduma hizo mpya za watu kulipia ili watumiaji maarufu wa Twitter wapate faida na Twitter pia ipate faida kwa kugawana nao faida ya subscriptions.