Msanii wa muziki nchini Tanasha Donna Oketch hatimaye amezungumza kuhusu video iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha Diamond Platnumz akikwepa busu lake wakiwa jukwaani kwenye tamasha la Tumewasha jijini Dar es Salaam.
Akijibu shabiki mmoja kwenye mtandao wa Instagram, Tanasha donna amesema kwamba watu kwenye mitandao ya kijamii wanaruhusiwa kufurahia tukio nzima kwani haoni kitu cha kuzungumziwa kwenye video hiyo.
Kauli yake inakuja baada ya shabiki yake kuweka ujumbe wa kumtetea, yenye maelezo kuwa alikuwa anajaribu kumunong’oneza kitu diamond Platnumz na wala sio busu kama wengi walivyodhani.
Ikumbukwe wiki hii, tanasha Donna amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kurudiana na baby dady wake.
Mwanamuziki huyo alitua nchini Tanzania Ijumaa wiki iliyopita, kumpeleka mtoto wake Naseeb Junior kukutana na baba yake baada kutoonana kwa miezi kadhaa.