Staa wa muziki nchini Tanasha Donna amefikisha zaidi ya followers millioni 3 kwenye mtandao wa Instagram.
Tanasha Donna ambaye anafanya vizuri na mkwaju wake wa Kalypso hakuficha furaha yake ya kufikisha jumla ya Wafuasi million 3.1 kwenye mtandao huo kwani ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwapa mashavu mashabiki wake kwa kumpa support kwenye shughuli zake za kimuziki ikizingatiwa kuwa sio jambo rahisi kushawishi watu kumfuatilia kwenye mitandao ya Kijamii
Kwa matokeo hayo Tanasha Donna anakuwa msanii wa kwanza wa kike nchini kuwa na followers wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram akifuatwa na Akothee aliye na followers million 2.6.