Mtangazaji wa Runinga moja nchini maarufu kama Hustle Goddes amemtuhumu msanii wa kike nchini Tanasha Donna kwa madai ya kukwepa kulipa deni ya huduma ambayo msanii huyo alipewa kipindi anaanda video ya wimbo wake wa “Kalypso.”
Akipiga stori na mchekeshaji wa humu nchini Eric Omondi mrembo huyo amesema licha ya marafiki zake kutoa huduma ya make up kwa Tanasha Donna, msanii huyo ameshindwa kulipa pesa zao kwani kila mara akiulizwa kuhusu deni hilo anaingiwa na jeuri.
Hata hivyo Tanasha Donna ameonekana kumjibu mrembo huyo kimafumbo kwa post picha yenye caption “Tanasha=Content,” ujumbe uliotafsiri na wajuzi mambo nchini kama ni kijembe kwenda kwa Hustle Goddess.
Ikumbukwe sio mara ya kwanza kwa Tanasha Donna kudaiwa kushindwa kulipa madeni kwani mapema mwezi mei mwaka wa 2020 alianikwa na baadhi ya wafanyibiashara wa nguo jiji nairobi baada ya kushindwa kulipa deni la shillingi 23100.