Mwanamuziki kutoka nchini uganda Fik Fameica kwa miaka kadhaaa sasa ana umaarufu wa kuwachumbia mastaa wenzake akiwemo Sheila Gashumba na Lydia Jazmine.
Wiki kadhaa zilizopita Rapper huyo aliachia collabo yake na Spice diana iitwayo Ready na kama njia ya kuutangaza wimbo huo wawili hao wamekuwa wakienda interviews mbali mbali wakiwa pamoja, jambo ambalo limeibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa muziki nchini uganda wengi wakihisi labda wanatoka kimapenzi.
Sàsa akiwa kwenye moja ya interview Spice diana amepuzilia mbali madai hayo na kusisitiza kwamba hawezi toka kimapenzi na rapa huyo kwani ukaribu wao ni wa kishkaji tu.
Ikumbukwe spice diana kwa muda sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na meneja wake Roger Lubega, taarifa ambazo mrembo huyo amekuwa akizikana na kudai kwamba meneja wake huyo ana familia, hivyo anamheshimu.