Rapa Soulja Boy kutoka Marekani ameripotiwa kufunguliwa mashtaka na mwanamke mmoja ambaye anadai kubakwa na rapa huyo kipindi anafanya kazi kama msaidizi wake.
Mwanamke huyo ambaye hakutaka kuanika jina lake, amefungua shtaka hilo kwenye Mahakama Kuu ya mjini Los Angeles dhidi ya Soulja Boy, shtaka ambalo limetaja makosa kama Kubakwa, Kushikiliwa na kufungiwa ndani kinyume cha sheria, lakini pia kufanyishwa kazi kwenye mazingira magumu pasi na kulipwa mshahara.
Baada ya kuanza kazi Disemba 2018, mwezi mmoja baadaye anadai Soulja Boy alianza kumtumia picha za Uume wake kwenye simu. Kitendo ambacho kiliashiria kwamba anataka mahusiano na mfanyakazi huyo ambaye hakuwa tayari na aliishia kupigwa hadi kupoteza fahamu mara kadhaa na kubakwa pia.
Shtaka hili linakuja ikiwa ni mwaka mmoja na miezi sita tangu Soulja Boy aachiwe huru baada ya kutumikia miezi mitatu kwenye kifungo cha miezi Nane kwa kukiuka mashtarti ya muda wa uangalizi kwenye shtaka lake la kubeba silaha yenye risasi hadharani mwaka 2014.