SHULE YA UPILI YA ST KEVINS MJINI LODWAR YAFUNGWA KWA MUDA

Shule ya upili ya St Kevins mjini Lodwar, Kaunti ya Turkana imefungwa kwa muda kutokana na mafuriko yanayoshuhudiwa kaunti hiyo baada ya mto Turkwel kuvunja kingo zake.

Akizungumza na wanahabari mjini Lodwar Mwalimu Mkuu wa shule ya Upili ya St. Kevins Thomas Lokuruka amesema hatua hiyo imetokana na madarasa na vyoo vya shule hiyo kusombwa na mafuriko siku chache zilizopita.

Aidha Lokuruka amewaondolea hofu wazazi walio na wanafunzi wa kidato cha nne shule humo kuwa uongozi wa shule hiyo utafanya kila liwezalo kuhakikisha watahiniwa wa kidato cha nne wanakalia mtihani wao wa kitaifa bila kizingiti.

Hata hivyo ametoa wito kwa washikadau wa elimu kuingilia kati na kusaidia shule ya upili ya St. Kevins na mahitaji ya msingi ili kuwasaidia wanafunzi wa kidato cha nne wanaojianda kufanya mtihani wao wa kitaifa.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts