SHIRIKA LA WORLD VISION LASAMBAZA MBUZI KWA MAKUNDI KADHAA ENEO LA SOOK, ENEO BUNGE LA KAPENGURIA

You are currently viewing SHIRIKA LA WORLD VISION LASAMBAZA MBUZI KWA MAKUNDI KADHAA ENEO LA SOOK, ENEO BUNGE LA KAPENGURIA

Shirika la World Vision linaendelea na harakati za kuwezesha Jamii ya Pokot Magharibi kujitegemea badala ya kusubiri misaada na usaidizi kutoka kwa wahisani na mashirika.

Kulingana na Teresa Cheptoo kutoka Shirika hilo chini ya idara ya kupinga ukeketaji akiwa katika eneo la Sook amesema, mpango wa kupeana Mbuzi kwa vikundi mbalimbali eneo hilo ni kukwamua jamii kuichumi kando na kupunguza umaskini.

Katika mazungumzo ya kipekee na Northrift Radio Cheptoo anahoji kuwa watafwatilia mpango huwo kuhakikisha Mbuzi waliopewa wanajamii inawafaa kando na kuitaka Serikali ya kaunti kuimarisha miradi sawia kuondoa umaskini na kustawisha jamii kiuchumi, kielimu na kimaendeleo.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.