SERIKALI YA KAUNTI YA TURKANA YAZINDUA MRADI WA MAJI, NAPUU

SERIKALI YA KAUNTI YA TURKANA YAZINDUA MRADI WA MAJI, NAPUU

Wakaazi wa  kaunti ndogo ya turkana ya kati wana kila sababu ya kutabasamu, baada serikali ya kaunti ya turkana kwa ushirikiano na mamlaka ya kuvuna na kuhifadhi maji nchini kuzindua mradi wa maji wa napuu viungani mwa mji wa lodwar.
Akizungumza alipozindua mradi huo mjini lodwar, gavana wa kaunti ya turkana josphat koli nanok amesema lengo la mradi huo ni kuwezesha upatikanaji wa maji ya kutosha maeneo yote ambayo yapo kaunti ndogo ya turkana ya kati kwa matumizi ya nyumbani na mifugo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mamlaka ya kuvuna na kuhifadhi maji nchini david nkedenyi amesema mradi huo ambao umegharimu  shillingi millioni 72  utawafaidi  zaidi ya wakaazi elfu ishirini na tano.
Hata hivyo gavana wa kaunti ya turkana josphat nanok amewataka waakazi wa kaunti ndogo ya turkana kati wanaoishi karibu na mradi wa maji wa napuu kuweka mikakati ya kulinda maji hayo ili yadumu bila kuchafuliwa kiholela

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts