Changamoto imetolewa kwa serikali Kaunti ya Turkana na ile Kitaifa kuwasaidia zaidi watu wenye ulemavu kwani wengi wao wanaishi kwenye lindi la umaskini.
Akizungumza alipopokea shehena ya chakula kutoka kwa washirika wa maendeleo, Afisa wa Idara ya huduma kwa jamii jimbo katoliki la Lodwar Mark Nakain amesema vita dhidi ya umaskini kwa watu wenye ulemavu havitashindwa iwapo sera na mipango ya kuwawezesha walemavu haitaweka na serikali.
Kauli sawa imetolewa na watu wenye ulemavu waliyofaidi na msaada wa vyakula ambapo wametoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kutoa msaada wa vifaa na vyakula kwa watu wenye ulemavu ili waweze kujikwamu kutoka kwa umaskini.
Hata hivyo Nakain ametumia fursa hiyo kuirai serikali ya kaunti ya Turkana kuanza kutoa elimu kwa wakaazi kuhusu homa ya Corona ambayo kwa sasa imetetemesha ulimwengu.
Kauli yake inakuja siku moja baada ya Waziri wa Afya kaunti hiyo Jane Ajele kudokeza kuwa serikali ya kaunti imepokea vifaa vya kupambana na homa ya Corona kwani tayari imetenga vituo 12 vya kushughulikia visa vyovyote vya Corona vitakavyoripotiwa kaunti yaTurkana.