SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI IMO MBIONI KUKAMILISHA MIRADI MUHIMU YA MAENDELEO.

You are currently viewing SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI IMO MBIONI KUKAMILISHA MIRADI MUHIMU YA MAENDELEO.

Serikali ya Kaunti ya Pokot Magharibi inatazamwa kwa kina na mawananchi kuelekea utekelezwaji wa miradi ya maendeleo hususan ujenzi wa Viwanda baada ya Gavana wa jimbo hilo Professor John Krop Lonyang’apuo kuahidi mwananchi kwenye manifesto yake huku muda ukiyoyoma kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu mwaka 2022.

Baada ya mipango ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa kiwanda cha maembe Wodi ya Lomut eneo bunge la Sigor kaunti ya Pokot Magharibi wiki jana siku ya ijuma, macho yote sasa yanaelekezwa kwa Kaunti hiyo wiki kesho mwezi huu katika uwekaji jiwe la msingi maeneo ya Kabichibich eneo bunge la Pokot Kusini kuzindua ujenzi wa kiwanda cha maziwa kwa faida ya wafugaji wa ng’ombe wa maziwa.

Mapema mwezi jana February, Mkurungenzi wa uwekezaji na vyama vya ushirika Kaunti ya Pokot Magharibi William Ntoina katika mzungumzo ya kipekee na North rift radio alitoa hakikisho kwamba miradi yote kwenye manifesto ya Gavana Lonyang’apuo itatekelezwa kabla ya kura za mwaka 2022 licha ya changamoto ambazo zitajitokeza kipindi kilichosalia cha utawala.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.