SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI IMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA WASHIRIKA WA MAENDELEO

Serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi imeahidi kushirikiana na washirika wa maendeleo kuboresha huduma za afya na elimu kaunti hiyo.

Akizungumza alipowapokea maafisa kutoka Marekani Gavana wa kaunti ya Pokot John Krop Lonyang’apuo amesema wanalenga kupanua kitengo cha kuwahifadhi watoto njiti kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kapenguria ili kukithi idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao.

Aidha Lonyang’apuo amesema wanalenga pia kuboresha miundo mbinu za shule zilizoko mpakani ili kuhakikisha watoto kutoka maeneo hayo wanapata elimu sawa na wenzao kutoka maeneo mengine ya nchi.

Kwa upande wake J Peters ambaye alikuwa mgeni wa Gavana wa kaunti ya Pokot Magharibi amesema wameriathia ombi la Gavana Lonyang’apuo la kuboresha huduma za afya na kuinua viwango vya elimu huku akiahidi kutoa msaada wowote wa kifedha kwa ajili ya kufadhili miradi ya maendeleo.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts