Serikali imetakiwa kukoma kuagiza maziwa kutoka mataifa ya kigeni na badala yake kuekeza nchini.
Mwanachama wa kamati ya Kilimo katika Bunge la Kitaifa Ferdinand Wanyonyi amesema kwamba wafugaji wengi wa ngombe wa maziwa hawajakuwa wakipata faida ya kutosha kutokana na bei duni.
Wanyonyi ambaye pia ni Mbunge wa Kwanza kaunti ya Trans- Nzoia amesema kwamba mataifa wanachama wa Afrika Mashariki kama vile Uganda linaelekea kuipiku Kenya kwa kuzalisha maziwa kutokana uwepo wa soko nzuri.