SENETA SAMWEL POGHISHO AWASUTA VIONGOZI WANAOEZA SIASA ZA PROPAGANDANA NA MIGAWANYIKO

SENETA SAMWEL POGHISHO AWASUTA VIONGOZI WANAOEZA SIASA ZA PROPAGANDANA NA MIGAWANYIKO

Seneta wa Kaunti ya Pokot Magharibi Samwel Poghisio amemsuta vikali  Mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing  kwa kutilia shaka uongozi wa gavana John Krop Lonyang’apuo, akisema anajitakia makuu kisiasa.

Akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa kanisa huko Sook, Eneo bunge la Kapenguria, Seneta Poghisio amemtaka mbunge huyo kukoma kueneza uvumi kuwa amekuwa miongoni mwa viongozi ambao wamekuwa wakishinikiza gavana wa kaunti hiyo akamatwe na makachero wa DCI kwa tuhuma za ufisadi.

Aidha Poghisio amemnyoshea  Pkosing kidole cha lawama kwa kuadaa wakaazi wa Kaunti ya Pokot Magharibi kuwa amechangia pakubwa kuletwa kwa miradi ya maendeleo kaunti hiyo ikiwemo ujenzi wa barabara ikizingatiwa kuwa mbunge huyo ni mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu uchukuzi.

Hata hivyo ameitaka serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi ikiongozwa na Gavana John Krop Lonyangapuo kuweka wazi kiwango cha pesa ambacho kilitolewa na wahisani kwa waathiriwa wa mkasa wa maporomoko ya ardhi iliyotokea mwaka jana maeneo ya Nyarkulian,Sebit,Parua na Mwino kaunti hiyo.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts