Kundi la muziki nchini Sauti Sol limesaini mkataba na kampuni ya Pace Africa kutengeneza spika ndogo za masikioni (EarBuds) ziitwazo PaceSol.
Sauti sol wametumia ukurasa wao wa Instagram kuwataharifu mashabiki wao kuhusu mpango wao wa kuja na bidhaa mpya ambazo zitawatambulisha kama kundi.
Kulingana na wakali hao wa ngoma ya Suzzana, PaceSol itakuwa ni bidhaa yao ya kwanza kwa ushirikiano na kampuni ya Pace Africa wakiwa na mpango pia wa kuzindua bidhaa nyingine za teknolojia kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Hata hivyo wamesema bidhaa za PaceSol zinalenga kuwahimiza wafrika kuwa wabunifu kwenye masuala ya ujarisilimali huku wakifurahia muziki wao.