Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand amesema ni mapema kwa klabu ya Liverpool kufikiria kumtimua kocha wake, Jurgen Klopp kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo kwa siku za hivi karibuni.
Ferdinand ametoa kauli hiyo kutokana na presha kubwa anayopata Klopp huku akibainisha kuwa upepo huo mbaya unaoikumba timu hiyo unatokana na majeraha ya muda mrefu kwa baadhi ya wachezaji wao tegemeo hasa wa safu ya ulinzi.
Aidha, nyota huyo wa zamani wa United amesema kuwa hana shaka na uwezo wa Klopp kwakuwa ameifikisha timu hiyo fainali ya Ligi ya Mabingwa mara mbili huku moja wakibuka kidedea kwa kutwaa ubingwa huo na taji Ligi Kuu ya England (EPL) walilolisubiri kwa muda mrefu.