Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Ringtone ametoa onyo kali kufuatia kuanzishwa kwa awamu ya pili ya kipindi cha Eric Omondi kiitwacho “Wife Material”.
Ringtone kupitia ukurasa wake wa Instagram, amepost video anayozungumzia kipindi cha mchekeshaji eric omondi ambacho kwa mujibu wake, kinawakosea heshima wanawake.
Ameeleza kuwa, Eric Omondi anaacha mabinti za watu wakimng’ang’ania kisa na maana anatafuta mke.
Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili, anasema kwamba atamwonya Eric Omondi mara tatu na ikiwa hatakatiza kipindi chake, atamwombea na kitu kibaya kitamtokea.
Ikumbukwe, awamu ya kwanza ya kipindi hicho kilihusu kina dada wa nchini Kenya na awamu hii ya pili inahusisha wanawake tisa, watatu kutoka kila nchi ya Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda na Tanzania.