RAYVANNY ATAMBULISHA LOGO RASMI YA LEBO YAKE YA MUZIKI

You are currently viewing RAYVANNY ATAMBULISHA LOGO RASMI YA LEBO YAKE YA MUZIKI
  • Post category:Burudani

Baada ya subira ya muda mrefu hatimaye mkali wa muziki wa Bongofleva Rayvanny ametujuza rasmi jina la record label yake inayotajwa kuwa na studio kali ndani yake kuliko label nyingine nchini Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rayvanny amepost picha yenye chapa ya lebo hiyo ambayo itajulikana kama Next Level Music na kisha kuandika “Ilikuwa ndoto Next Level Music #NLM”.

Staa huyo anayefanya vizuri na Album yake Sound from Africa anakuwa kati ya wasanii wachache wanaomiliki lebo nchini Tanzania. Lakini pia anakuwa msanii wa kwanza kwenye lebo ya WCB kumiliki lebo yake binafsi huku akiendelea kufanya kazi chini ya leo hiyo.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa