RAPA TEKASHI 69 AFUNGULIWA MASHTAKA,ADAIWA KUTOWALIPA FEDHA WALINZI WAKE.

You are currently viewing RAPA TEKASHI 69 AFUNGULIWA MASHTAKA,ADAIWA KUTOWALIPA FEDHA WALINZI WAKE.
  • Post category:Burudani

Kampuni ya Metropolitan Patrol imemfungulia shtaka rapa Tekashi 69 kutoka marekani kwa madai ya kutolipa fedha za ulinzi. 

Mwaka 2018, kampuni hiyo ilimpatia rapa huyo walinzi (bodyguards) kwa makubaliano ya kuwatumia kwa siku 11 kipindi ambacho anawindwa mara baada ya kuwa-snitch waliokuwa washkaji zake kwenye kesi iliyokuwa ikiwakabili pamoja.

Makubaliano yao yalimtaka Tekashi 69 kuilipa kampuni hiyo ya ulinzi kiasi cha shillingi millioni 8.2 lakini pia Walimpatia gari lenye usalama wa kutosha pamoja na vifaa vyote vya ulinzi.

Kwa mujibu wa TMZ, Metropolitan Patrol wamefungua shtaka hilo la madai wakieleza kwamba wanamdai kiasi cha shillingi millioni 8.2 na hadi leo amekuwa akipiga chenga.

Aidha wameiomba mahakama kusaidia kufanyika kwa malipo hayo ambayo wameongeza na pesa ya usumbufu na sasa kiasi wanachotaka ni takriban shillingi millioni 20.6. 

Mwanasheria wa Tekashi 69 amejibu shtaka hilo kwa kusema, kampuni ya MTA Bookings ndiyo inahusika na malipo hayo na sio mteja wake kwani wao ndio waliajiriwa kwa ajili ya kufanya shughuli za booking.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa