Rapa Quavo wa kundi la Migos amemuongeza meneja Scooter Braun kwenye menejimenti yake. Scooter atashirikiana na Danny Zook ambaye ni meneja wa Migos katika kumkuza Quavo kwenye kazi zake binafsi.
Scooter Braun ni miongoni mwa meneja wakubwa nchini Marekani na anafanya kazi na wasanii wenye majina duniani akiwemo; Justin Bieber, Ariana Grande, Demi Lovato na YG.
Kundi la Migos litaendelea kuongozwa na Zook pamoja na Quality Control.