Rapa na Mwigizaji Ice Cube kutoka Marekani ameishutumu kampuni ya Warner Bros kuwa ndio inazuia kutoka kwa muendelezo wa filamu za FRIDAY.
Akitumia Hashtag isemayo Free Friday Ice Cube amesema kampuni hiyo imekataa kutoa muendelezo wa filamu hiyo ambayo ilifanya vizuri kwenye soko la filamu duniani.
Filamu ya kwanza ya Friday ilitoka April 26, mwaka wa 1995 na kuingiza takriban billioni 2.9 duniani kote, ilifuatiwa na ‘Next Friday’ iliyotoka mwaka wa 2000 na ya mwisho ilikuwa ‘Friday After Next’ ambayo ilitoka mwaka wa 2002.