Rapa kutoka nchini Uganda GNL Zamba ametia nia ya kugombea wadhfa wa urais wa chama cha wanamuziki nchini humo ambao ulikuwa unashikiliwa na msanii Ykee Benda.
Akiwa kwenye moja ya interview Zamba ameweka wazi mipango ya kuboresha tasnia ya muziki nchini uganda huku akisema kwamba anataka kuwasaidia wasanii jinsi ya kuingiza mkwanja kupitia kazi zao bila ya kutumbuiza kwenye matamasha ya muziki.
Zamba amesema amekuwa akiishi kupitia mapato ya muziki wake kwa njia ya mtandao na nataka kuwahamasisha wasaniii wa uganda ambao wamekuwa na mazoea ya kuomba msaada kila mara kutoka kwa serikali jinsi ya kupata pesa kwa njia ya mtandao.