Rapa Eazi Money kutoka nchini Jamaica amemsuta vikali msanii nguli wa Reggae nchini humo Jah Cure kwa hatua ya kushindwa kumaliza mashairi ya collabo yao aliyolipwa miaka minne iliyopita.
Kwa mujibu wa Eazi Money ambaye hapa kati alishare baadhi ya jumbe za vitisho kutoka kwa Jah Cure mitandaoni, hajefurahishwa na jinsi msanii huyo wa reggae alivyomtishia maisha, hivyo amewataka wadau wa muziki nchini Jamaica wamsaidia ili Jah Cure amlipe pesa zake kama suala la collabo limeshindikana.
Hata hiyo Eazi Money amewashukuru mashabiki wake na wanablogu kwa kueneza chapisho lake na kuwafanya watu wafahamu kile Jah Cure amemtendea huku akitawataka wakae mkao wa kula kwa EP yake iitwayo “Reggae Vibe & Summer Nights” ambayo itaachia rasmi tarehe 28 mwezi huu wa Februari.