Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amepeleka kampeni za kupigia debe mpango wa maridhiano wa BBI katika kaunti ya Turkana.
Akizungumza katika Bustani ya Moi mjini Lodwar Waziri Mkuu huyo wa zamani amesema ripoti ya BBI ina manufaa makubwa kwa Wakenya endapo itaidhinishwa kwani itafanikisha kubuniwa kwa ajira na upanuzi wa biashara.
Aidha,amewataka vijana na kina mama kuunga mkono ripoti hiyo,huku akisema sera za BBI zitasaidia kuinua maisha ya vijana na kina mama humu nchini, kinyume na matamshi yanayotolewa na viongozi wanaopinga mchakato huo.
Raila ambaye yupo kwenye ziara ya siku ya tatu kaunti ya Turkana amesisitiza kwamba BBI itasitisha ufisadi nchini pamoja na kuchangia uchaguzi huru na amani.